102/2

KISWAHILI

KARATASI

LUGHA

OCT/NOV 2006

1. UFAHAMU

Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali

Ulimwengu unapaswa kuzuka na mbinu za Kulitadarukia tatizo la umaskini ambao unakwamiza juhudi za maendeleo. Umaskini unaoyakabili mataifa yanayoendelea. Unayatosa kwenye dhiki kubwa huku mataifa ya kimagharibi yakitpiga hatua kubwa kimaendeleo. Ufa uliopo baina ya mataifa yanayoendelea na yalo yaliyoendelea kama vile Marekani, nchi za Ulaya na Ujapani unapanuka kila uchao.

Vyanzo vya umaskinin huu ni anuwai mathalan, ufusadi, uongozi mbaya, turathi za kikoloni, uchumi kuegemea mvua isiyotabarika, idadi ya watu inayoupik uwezo wa uchumi wa taifa linalohusika na ukosefu wa nyenzo na amali za kuwakwamua raia kutoka lindi la umaskini. Ukosefu adimu za ajira huchangia pia katika tatizo hili.

Jamii ya ulimwengu inapaswa kuelewa kuwa umaskini unaoathiri nchi Fulani una athari pan asana. Uvunigu unaotokana na umaskini unaweza kuweza kuwa mboji ambako matendo ya kihalifu ili kujinasua kutoka dhiki ile. Hii inaweza kuwa mbegu ya kuatika maovu kama ugaidi na uhalifu wa kila aina.

Mataifa ya magharibi yanapaswa kuyaburai madeni mataifa yanayoendelea kama njia mojawapo ya kupambana na umaskini. Asilimia kubwa ya pato la kitaifa katika mataifa mengi hutumika kuyalipa madeni hayo. Katika hali hii inakuwa muhali kwa mataifa hayo kujikwamua kutokana na pingu za umaskini. Njia nyingine ni kustahabu kutoa ruzuku za kimaendeleo badala ya mikopo kwa nchi zinazoendelea.

Kwa upande wake, mataifa yanayoendelea yanapaswa kuibuka na mikakati bora ya kupambana na umaskini. Ni muhimu pawepo na sera zinazotambua ukweli kuwa asilimia kubwa ya raia wa mataifa hayo ni maskini. Pana dharural ya kuzalisha nafasi za ajira, kupanua viwanda hususan vinavyohusiana na zaraa ambayo ni tegemeo kuu la mataifa mengi, kuendeleza elimu na kuimarisha miundo msingi. Ipo haja pia ya mataifa haya kuhakikisha kuwa mfumo wa soko huru unaotawala ulimwengu sasa huishii kuwa chanzo cha kufa kwa viwanda asilia na kuendeleza masikini zaidi. Kwa ufupi, maamuzi yote ya sera za kiuchumi lazima yazingatie uhalishi wa maisha ya raia wa mataifa hayo.

a) Kwa nini umaskini umetamalaki katika mataifa yanayoendelea? (alama 4)

b) Madeni yana athari gani kwa mataifa yanayoendelea? (alama 2)

c) Ni mapendekezo yapi ambayo mwandishi anatoa kwa mataifa machanga kuhusu

utatuzi wa tatizo la umaskini?

d) Mfumo wa soko huru una mathara gani kwa mataifa machanga? (alama 2)

e) Ukirejea kifungu, eleza maana ya:

i) Kulitadarukia

ii) Kuatika

iii) Kuyaburai madeni

2. MUHTASARI

Ajira ya watoto ni tatizo sugu linalokumba ulimwengu wa sasa , hasa katika nchi zinazozoendelea. Jambo la kusikitisha ni kwamba hivi ndivyo ilivyo katika nchi nyingi za ulimwengu huu. Kuna idadi kubwa ya watoto wanaoajiriwa katika nyanja mbalimbali za jamii. Zipo sababu nyingi zinazowasukuma watoto kutafuta ajira barani Afrika kwa mfano, familia nyingi huishi maisha ya ufukara hivi kwamba hushindwa kuyatimiza mahitaji muhimu hususan kwa watoto. Kapanda kwa gharama ya maisha kunazidisha viwango vya umaskini. Ukosefu wa lishe pia huwafanya watotto kutoroka nyumbani kutfuta ajira. Janga la UKIMWI limesababisha kuwepo kwa idadi kubwa ya mayatima wanaoshia kutafuta ajira ili kuyakimu maisha. UKIMWI umezifanya nyingi pia kuwaondoa watoto shule ili waweze kuajriwa kwa lengo la kuanzisha pato la familia hizo. Watoto wengine hutoroka makwao kwa sababu ya maonevu. Maonevu haya ni kama vile kupigwa, kutukanawa kila wakati, kunyanyaswa kijinsia na kadhalika. Huko nje hutaabishwa kimwili na kiakili. Hufanyishwa kazi za sulubu zenye malipo duni au wasilipwe kabisa. Hili huwasononeshe na kuathiri afya yao.

Uundaji wa Umoja wa Afrika hivi majuzi ni hatua muhimu ya kushughulikia matatizo ya

Afrika kama vile ajura ya watoto, kuzorota kwa miundo msingi, magonjwa, njaa,

umaskini, ufisadi na ukabila. Katika kushughulikia haki za watoto, nchi za Afrika hazina

budi kuzingatia masharti yalivyowekwa na Umuja wa Mataifa kuhusu haki za watoto.

Nchi nyingi za Afrika ziliidhinisha mkataba wa marsharti hayo ikiwemo inchi ya Kenya.

Nchi hizi basi lazima zishughulikie haki za watoto kupitia sheria za nchi. Watoto ni rasilimali muhimu na ndio tumaini la kuwepo kwa kizazi cha binadamu.

a) Eleza mambo yote muhimu anaazungumzia mwandishi katika aya ya kwanza

(maneno 45-50) (alama 7, 1 ya utiririko)

Matayarisho

Jibu

b) Bila kubadilisha maana aliyokusudia mwandishi, fupisha aya mbili za mwisho (maneno 50-55) (alama 8, 1 ya utiririko)

Matayarisho

Jibu

3 MATUMIZI YA LUGHA

a) Tunga sentensi inayodhihirisha matumizi ya ngeli ya I – I (alama 1)

b) Changanua sentensi ifuatayo ukitumia mchoro wa matawi:

Mkulima mzembe amepata hasara (alama 4)

c) Onyesha viambishi awali na tamati katika kitenzi: Alimchezea (alama 3)

d) Taja sauti mbili zinazotamkiwa midomoni (alama 2)

e) Kanusha sentensi ifuatayo:

Ningalikuwa na pesa ningalinunua nyumba (alama 2)

f) Kitenzi fumbata kiko katika hali (kauli) ya (alama 1)

g) Tunga sentensi ukitumia kielezi cha

i) Wakati (alama 1)

ii) Mahali (alama 1)

h) Andika sentenzi zifuatazo kulingana na maagizo uliyopewa (alama 1)

i) Mhunzi mrefu alishinda tuzo (Anza kw: tuzo… (alama 1)

ii) Mwanafunzi huyu anasoma Kifaransa. (Anza kwa kiashiria kisisitizi)

i) Sentensi hizi ni za aina gani?

i) Lonare anatembea kwa kasi. (alama 1)

ii) Halima anaandika hali Ekomwa anasoma (alama 1)

j) Tunga sentensi moja ukitumia neon “seuze” (alama 1)

k) Bainisha Kirai Nomino na Kirai Tenzi katika sentensi:

Jirani mwema alinipa chakula (alama 2)

i) Unda nomino kutokana na vitenzi:

i) Chelewa (alama 1)

ii) Andika (alama 1)

m) Onyesha hali katika sentensi zifuatazo:

i) Henda mvua ikanyesha leo. (alama 1)

ii) Miti hukatwa kila siku duniani. (alama 1)

n) Unganisha sentensi zifuatazo ukitumia neon “japo”

i) Selina alijitahidi sana .

(ii) Selina hakushinda mbio hizo (alama 1)

o) Andika kinyume cha:

Mwise alikunja nguo alizokuwa ameanika (alama 2)

p) Sahihisha sentensi:

Mtoto ambaye niliyemsomesha ameasi jamii (alama 1)

q) andika katika msemo wa taarifa. “Sitathubutu kumpa pesa zangu” Mkolwe alisema. (alama 2)

r) Tunga sentensi kuongyesha tofautu kati ya vitate vifuatavyo (alama 2)

Suku na zuka

s) Eleza matumizi ya ritifaa katika: ‘N” shamchukua (alama 2)

t) Andika udogo na ukubwa wa neno ‘kiti’ (alama 2)

u) Eleza matumizi ya “na” katika sentensi: (alama 2)

Sofia na Raeli wanaandaliwa chai na mpishi

4 ISIMU JAMII

Soma kifungu kifuatacho ujibu maswali yanayofuata.

Kwa mujibu wa sheria kifungu nambari 3 sehemu ya A ya sheri za nchi, umepatikana na hatia ya kutatiza utulivu wa raia wapenda amani kwa kuwatusi na kutisha kuwapiga.

Kiongozi wa mashtaka amethibitisha haya wa kuwaleta mashahidi ambao wametoa ushahidi usiotetereka kuhusu vitendo vyako katika tukio hilo. Korti hii imeonelea una hatia na imeamuru ufungwe jela kwa muda wa miaka miwili bila faini ili liwe funzo kwako na kwa wenzako wenye tabia kama zako. Una majuma mawili kukata rufani.

a) Lugha iliyo katika kifungu hiki hutumika katika muktadha upi? (alama 1)

b) Toa ushaidi wa jibu lako (alama 3)

c) Zaidi ya sifa zilizo katika kifungu hiki, eleza sifa zingine sita za matumizi ya ligha katika muktadha huu. (alama 6)

 

More High School Past Papers