KNEC kiswahili 2009 past paper

Exam year:2009

High school Past papers

102/1

Kiswahili

Karatasi ya 1

INSHA

OCT/NOV. 2009

SAA 1 ¾

INSHA YA LAZIMA

1. Umealikwa kitongojini mwenu kama mgeni wa heshima katika hafla ya kuxindua kundi la wasanii wa Kikwetu. Andika hotuba utakayotoa y kuonyesha umuhimu wa sanaa na michezo.

2. “Utalii una madhara mengi kuliko faida hapa nchini.” Jadili.

3. Samaki huanza kuoza kichwani.

4. Andika insha itakayomalizikia kwa: Hapo ndipo nilipotambua kuwa kama maswala yao hayatashughulikiew kwa dhati, vijana ni kama bomu ambalo liko tayari kulipuka wakati wowote.

1. UFAHAMU

Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali.

Wanasaikolojia wanabainisha kati ya sehemu mbili kuu katika akili ya binadamu: Ung’amuzi na ung’amuzibwete. Ung’amuzi ni sehemu ya ubongo ambayo kimsingi hupanua na kudadavua yanayotendeka hususan mchana. Ung’amuzibwete ni kibinimethali chake; hufanya kazi wakati binadamu anapolemazwa na usingizi. Baadhi ya mambo anayoshuhudia binadamu mchana yanaingia kwenye ung’amuzibwete wake na kutokeza katika ndoto zake usiku.

Kwa mujibu wa mawazo ya Sigmund freud, mwanasaikolojia wa jadi anayechukuliwa nawengi kama mwasisi wa taaluma ya saikolojia, mambo yanayopatikana katika unga’amuzibwete mambo yana sifa hasi. Freud alidahili kuwa binadamu huyaficha na kuyabania kwenye ung’amuzibwete mambo ambayo hawezi juyasema kadamnasi. Alieleza kuwa matamanio yasiyokubalika, makatazo ya jamii, fikra na kauli zilizoharamishwa na miko ya kijamii hubanwa katika ung’amuzibwete. Shehena hiyo ndiyo inayochipuza kwa njia ya ishara za ndoto, mitelezo ya kauli, yaani maneno au kauli zinazotukoka bila wenye kukusudia, ishara na lugha ya kitamathali katika uandishi wa kibunifu na kadhalika.

Ung’amuzibwete un uwezo mkubwa wa kuathiri matendo ya binadamu. Huu ndio msingi unaowafanya wanasaikolojia wengi, akiwepo freud, kusema kuwa tajiriba ya motto inaweza kufichwa kwenye sehemu hiyo na hatimaye kuishia kutokeza katika utu uzima wake. Kwa kuwa tunapoingiliana na binadamu wenzetu kila siku tunayang’amuzibwete unapotawala binadamu wenzetu watashindwa kutuelewa. Hii ndiyo hali anayokuwa nayo mwendawazimu. Ung’amuzibwete wake hutawala. Sisi tunaotawaliwa na ung’amuzi tunashindwa kumwelewa; naye bila shaka anashindwa kutuelewa.

Carl Gustav Jung, aliyewahi kuwa mwanafunzi wa Freud, aliupinga mwelekeo wa Freud wa kuungalia ung’amuzibwete kama jaa la mawazo mabaya, matamanio, nia, fikira tuli na dhana ambazo ni hasi. Jung alizuka na dhana mbili muhimu: Ung’amuzibwete wa kibinafsi na un’gabuzibwete jumuishi. Alisema mambo, fikra na uzoefu wowote mbaya unaomuhusu mtu binafsi . Dhana ya ung’a muzibwete jumuishi aliitumia kuelezea sehemu ya akili ya binadamu ambayo inamfanya ayatende matendo Fulani kama binadamu wenzake licha ya tofauti zao kiwakati na kijiografia. Kwa mfano, binadamu wengi wana sherehe za kuzaliwa motto, kuoza, ibada au mviga unaohusiana na kifo licha ya tofauti zao. Jung alisema kuwa kinachochochea hali hii ni urithi Fulani wa kila mwanadamu. Urithi huo unapatikana katika ung’amuzibwete jumuishi.

Upo mwafikiano kati ya wataalamu hawa wawili kuwa ung’auzibwete una uwezo wa kuathiri ung’amuzi matendo ya binadamu ya king’amuzi. Wanasaikolojia wanashikilia kuwa binadamu hawezi kukamilika bila kuzihusisha sehemu zote mbile kwa sababu zinaathiriana.

a) Kwan in ung’amuzibwete unaelezwa kama kinyme cha ung’amuzi?

(alama 2)

b) Eleza mtazamo wa Freud kuhusu ung’amuzibwete. (alama 3)

c) Kwa mujibu wa Freud yaliyomo kwenye ung’amuzibwete hudhihirika vipi?

(alama 4)

d) Eleza tofauti ya mawazo kati ya Sigmund Freud na Carl Gustav Jung.

(alama 4)

e) taja hoja inayowafungamanisha Jung na Freud. (alama 2)

2. MUHTASARI

Utaifa ni mshikamano wa hisia zinazowafungamanisha watu wanaoishi katika taifa moja. Taif huundwa na watu wanaoishi katika nchi moja na ambao wanajitambua kisiasa kama watu wenye mwelekeo, mwono na hatima sawa. Utaifa umejengwa kwenye hisia za mapenzi kwenye hisisia za mapenzi kwa nchi na utambuzi wa kwamba rangi, cheo, hadhi, eneo, kabila au tofauti nyinginezo baina ya watu wanaoishi katika nchi moja si sbabu ya kuwatenganisha.

Nchi moja huweza kuwa na watu wa makabila tofauti, wenye matabaka ya kila nui na mawazo ainat. Watu hao wanapotambua kuwa kuna sherisi nyinyine inayowaunganisha kama fahari ya kuwa watu waochi hiyo, falsafa na imani sawa ambayo ishara yake kuu ni winbo wa taifa na kuwa tofauti kati yao muhimu huwa wamefikia kuunda taifa.

Mhili mkuu wa utaifa ni uzalendo. Uzaleno ni mapenzi makubwa aliyo nayo mtu kwa nchi yake. Malezi haya ndiyo yanyoongoza matendo yake, matamanio yake, mawazo yake, itikadi yake mwonoulimwengu wake na muhimu zaidi mkabala wake kuihusu nchi yake na hatima ya nchi yenywe. Uzalendo ni nguzo muhimu sana ya taifa. Mzalendo hawezi kuyatenda mambo yanayoweza kuletea mkama nchi yake.

Matendo ya mzalendo huangazwa na mwenge wa mema anayoitakia nchi au taifa lake. Hawezi kushiriki kwenye harakati na amali ambazo zinahujumu au kufumua mshikamano wa taifa zima au kutawaliwa na kitiba cha kutaka kujinufaisha yeye mwenyewe au jamii yake finyu. Matendo ya mzalendo wa kitaifa yanaongozwa na mwelekeo wa kuiboresha nchi yake. Swali linalomwongoza mtu huyo ni: nimeifanyia nini nchi yangu au taifa lahgu? Alhasili mtu anayeipenda nchi yake hawezi kuongozwa na umero wa kibinafsi tu wa kujilimbikia mali, ujiri au pesa. Yuko radhi kuhasirika kama mtu binafsi ili taifa au nchi yake inufaike.

Utaifa ni mche aali ambao unapaliliwa kwa uzalendo, kuepuka hawaa za nafsi, kusinywa na taasubi za kikabila na kuach tama ya kujinufaiha. Hali hiyo inapofikiwa, hatima ya wanajamii wa taifa linahusika huwa nzuri na mustakabali wao na wa vizazi vyao huwa wa matumaini makubwa.

a) Dondoa sifa kuu za utaifa. (maneno 40- 50) (alama 6, 1 ya mtiririko)

matayarisho.

Jibu

b) kwa kutumia maneno kati ya 60-70, onyesho misingi ya kumtathmini mzalendo.

(alama 9, 1 ya mitiriko)

Matayarisho .

Jibu

3. MATUMIZI YA LUGHA

a) andika sentensi mbili zifuatazo kama sentensi moja kwa kutumia kiwakilishi kirejeshi.

i) duka la Bahati lina bidhaa nyingi

ii) Juma anafanya kazi katika duka la Bahati. (alama 2)

b) i) Eleza matumizi mawili ya kiambishi –ji- (alama 2)

ii) tunga sentensi moja kuonyesha moja ya matumizi hayo.(alama 2)

c) Tumia visawe vya maneno yaliyopigwa mstari kuandika tena sentensi ifuatayo:

Ukuta umemweumiza mvulana alipokuwa akiuparaga (alama 3)

d) chora vielelezo matawi vya sentensi ifuatayo:

Bakari, Roda na Hirsi wamefurahi kupita mtihani. (alama 4)

e) Tambua sauti ambazo si za ufizi katika sauti hizi.

M, t, n, z, gh. (alama 1)

f) Tunga sentensi sahihi ukitumia –fa- katika hali ya mazoa. (alama 2)

g) Onyesha kwa kupiga mstari iliko shadda katika maneno mawili yafuatayo:

i) Malaika

ii) Nge (alama 2)

h) Eleza maana mbili za sentensi:

Kiharusi chake kimewaitia hofu. (alama 2)

i) tunga sentensi ukitumia kielezi cha jinsi cha nomino ifuatayo:

Uganda (alama 2)

j) Bainisha sentensi sahili zilizo katika sentensi mseto ifuatayo:

Hamali ambaye ameugua alisema kuwa angekwenda hospitali jana

(alama 3)

k) Andika ukubwa wa sentensi:

Ndovu wa Kiafrika ameharibu kichaka (alama 2)

I) Iandike tena sentensi ifuatayo bila kutumia vitenzi visaidizi

Wachezaji huenda wakawa wanaweza kushinda mchezo wa leo.(alama 2)

m) andika kw msemo halisi: Baba alipotuuliza kama tungependa kwenda Mombasa wakati wa likizo tulimjibu kwamba tulitaka kwenda Kisumu kwa kuwa tulikuwa hatujaliona Ziwa Victoria. (alama 3)

n) Huku ukitoa mifano mwafaka onyesha matumizi mawili ya kinyota(*) katika sarufi ya Kiswahili. (alama 3)

o) Kanusha sentensi ifuatayo:

hapo napo ndipo nitakapo. (alama 1)

p) andika kinyume cha:

furaha amehamia mjni. (a lama 1)

q) andika maneno yafuatayo katika kauli zilizoonyeshwa katika mabano

Neon Kauli Jibu

i) Imba (tendesha)……………………………………

ii) choka (tendea) …………………………………………

4. ISIMUJAMII

Eleza majukumu matano matano matano ya Kiswahili kama lugha ya Kitaifa na Kimataifa. (alama 10)

102/3

KISWAHILI

KARATASI YA 3

FASIHI

OKT./NOV. 2009

SAA 2 ½

RIWAYA

S.A MOHAMED: UTENGANO

1. Lazima

“ Katu asingajitia kibuibui na kutanga na njia. Lo, kachoshwa na shimiri za baruti anazoshindiliwa moyoni mwake.”

a) eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)

b) taja na ufafunue tamathali ya usemi iliyotumika katika dondoo hili

(alama 4)

c) Eleza umuhimu wa kisa kinachorejelewa na dondoo. (alama 4)

d) kwa kurejelea matukio mengine katika riwaya ya Utengano, fafanua maudhui

mawili yayoashiriwa na dondoo hili. (8 mks)

USHAIRI

Jibu swali la 2 au la 3

2 Soma shairi kisha ujibu maswali yanayofuata:

KIBARUWA: Abdilatif Abdalla

Kwenye shamba hilo kubwa asilani hakunyi mvuwa!

Ni kwa mitilizi ya jasho langu ndiyo hunweshezewa

Kwenye shamba hilo kubwa sasa imeshaiva kahawa

Na bunize ni matone ya damu yangu niliyotowa

Ndipo mte ukatipuza!

 

Buni hiyo itakaangwa buni hiyo itapondwapondwa

Buni hiyo itasagwa na buni hiyo itafyondwafyondwa

Bali itabaki nyeusi kama ngozi yangu Kibaruwa

Waulize ndege kwa nyimbo nyanana watutumbuizao

Iulize na mito kwa furaha maji itiririkao

Uulize na upepo mkali kwa ghadhabu uvumao-.

Viulize: Ni nani araukaye na mapema kuzitema mbuga na kuzilaza?

Viulize: Ni nani akweaye minazi tangu kuchapo hadi lingiapo giza?

Viulize: Ni nani abebeshwaye mizigo hadi maungo yakageuka shaza?

Halfuye hana faida moja apatay wala malipo yanayotosheleza-

Isipokuwa kusundugwa na kutupiwa matambara na vyakula viliyooza?

Viulize: Ni nani huyo ni nani!

Viulize: Ni nani aliyemaye mashamba na kuyapoliliya?

Na mimea kochokocho ikajaa kwa uzito ikajinamiya?

Hatimaye nani atajirikaye mali yakammiminikiya

Akatoa na kitambi kama mja mzito wa miezi tisiya

Na akaongeza magari na wanawake kutoka na kuingiya?

Viulize: Ni nani huyo nani1

Na hao ndege kwa nyimbo nyanana watutumbuizao

Nayo hiyo mito kwa furaha maji itirikao

Na huo upepo mkali wenye ghadhabu uvumao

Vyote hivyo vitatu vitakujibu kawa umoja wao

“Ni Kibaruwa Manamba ndiye mtendaji hayo!”

a) Eleza dhamira ya shairi hili. (alama 2)

b) Kwa kutoa mifano, eleza aina mbili za idhini ya kishairi

alizotumia mshairi (alama 4)

c) kwa kurejelea ubeti wa tatu taja na ueleze tamathali ya usemi na mbinu ya

kimuundo mshairi (alama 4)

 

d) Huku ukitoa mifano, eleza kwa kifupi mwelekeo wa mshairi kuhusu vibarua. (alama 4)

e) andika ubeti wa tano katika lugha ya nathari (alama 4)

f) Onyesha utata wa maana katika matumizi ya Kibaruwa Manamba (alama 2)

3. Soma shairi hili kisha ujibu maswali yayofuata:

Kila Mchimba Kisima

Musa Mzenga

1. Tenda utendapo tendo, tenda tendo kwa hekima,

Lindamane mwenendo, sawa na yakio kalmia,

Kalmia yenye upendo, kufurahisha mtima,

Kila mchimba kisima, budi hungia mwenyewe.

2. Utendapo la faraja, tendo ni yako salama,

Ya kukupa kila tija, na ushindi wa daima,

Upate njema daraja, duniani na kiyama,

Kila mchimba kisima, budi hungia mwenyewe.

 

3. Utendapo la miuja, tendo ni yako nakama

Ya kukutia harija, hasara kukuandama,

Usione afuwaja, mwanza ajue heshima,

Kila mchimba kisima, budi hungia mwenyewe

4. Nakwambia uelewe, pulika ninayosema,

Si ari ya mwenginewe, kumuonya kwa lazima,

Mtu hufunza mwanawe, Kwanza ajue heshima,

Kila mchimba kisima, budi hungia mwenyewe.

 

5. Nisipokwambia wewe, kukufunza kila jema,

Kusudi nikuongowe, uepukwe na tujuma,

Matusi ndimi nipawe, ila na kila lawama,

Kila mchimba kisima, bundi hungia mwenyewe

 

6. Hii si heri ujuwe, matusi kuigandama,

Hadhi usiniuzuwe, hamithilishwa na nyama,

Fikiri moyo utuwe, nikupapo taaluma

Kila mchimba kisima, budi hungia mwenyewe.

 

7. shika tena utambuwe, wasia huu ni mwema

Matendo usipunguwe, mazuri kutenda hima,

Yatende ubarikiwe, upawe na taadhima

Kila mchimba kisima, budi hungia mwenyewe.

8. Yakupasa uchunguwe, kila jambo kulipima

Upime ufafanuwe, mambo yote kwa alama

La kuwaka ulijuwe, pia lipi la kuzima,

Kila mchimba kisima hungia mwenyewe.

 

a) Eleza maudhui ya shairi hili. (alama 4)

b) Ujumbe unaowasilishwa katika shairi hili una hadhira lengwa tatu. Zitaje na utoe mifano. (alama 6)

c) Eleza umuhimu wa kipokeo kinachotumiwa katika shairi hili

(alama 4)

d) Andika ubeti wa tano kwa lugha ya nathari. (alama 4)

e) Eleza maana ya msamiati ufuatao kama ulivyotumiwa katika shairi:

i) afuwaja

ii) taaluma (alama 2)

More High school Past Papers