102/1

KISWAHILI

Karatasi ya 1

INSHA

Okt./Nov. 2012

Muda: Saa 1 ¾

THE KENYA NATIONAL EXAMINATION COUNCIL

Kenya Certificate of Secondary Education

KISWAHILI

Karatasi ya 1

INSHA

Muda: Saa 1 ¾

102/1 Kiswahili P1 – Insha

Wednesday – 8.00 am – 9.45 am

07/11/12 (1st Sesion)

Maagizo

 1. Andika insha mbili. Insha ya kwanza ni ya lazima
 2. Kisgha chagua insha nyingine moka kati ya hizo tatu zilizobakia
 3. Kila insha isipungue maneno 400
 4. Kila insa in alama 20
 5. Karatasi hii ina kurasa 2 zilizopigwa chapa
 6. Watahiniwa ni lazima wahakikishe kuwa kurasa zote za karatasi hii zimpigwa chapa sawasawa na kuwa maswali yote yamo.

1. Lazima:

Wewe ni mkuu wa Baraza la Wanafunzi shuleni mwenu. Kumekuwa na visa vya wanafunzi kukiuka sheria za shule. Andika kumbukumbu za mkutano wa baraza hili uliofanyika kujadili suala hili.

2. Anidka insha kuhusu umuhimu wa vijana katika kuimarisha mshikamano wa kitaifa.

3. Andika insha inayobainisha maana ya methali: Chombo cha kuzama hakina usukani.

4. Tunga kisa kinachoanza kwa maneno yafuatayo:

Nilijaribu kuyafumbua macho yangu yaliyojaa uchovu kutokana na malimbikizoya usingizi…

Jina………………………………………………… Nambari………………../…………

102/2 Sahihi ya Mtahiniwa………………

KISWAHILI

Karatasi ya 2 Tarehe………………………………

Okt. Nov. 2012

Muda: Saa 2 ½

THE KENYA NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL

Kenya Certificate of Secondary Education

KISWAHILI

Karatsi ya 2

LUGHA

Muda: Saa 2 ½

Maagizo

 1. Andika jina lako na nambari yako ya mtihani katika nafasi ulizoachiwa hapo juu.
 2. Tia sahihi yako kisha uandike tarehe ya mtihani katika nafasi ulizoachiwa hapo juu.
 3. Jibu maswali yote
 4. Majibu yote yaandikwe katika nafasi ulizoachiwa katika kijitabu hiki cha maswali
 5. Usitoe ukurasa wowote kutoka kwenye kijitabu hiki
 6. Karatasi hii ina kurasa 12 zilizopigwa chapa
 7. Watahiniwa ni lazima wahakikishe kwamba kurasa zote za karatasi hii zimepigwa chapa sawasawa na kuwa maswali yote yamo.

102/2 Kiswahili P2 – Lugha

Wednesday 10.45 am – 1.15 pm

07/11/2012 (2nd Session)

Kwa matumizi ya mtahini pekee

Swali Upeo Alama
1 15
2 15
3 40
4 10
JUMLA 80

1. UFAHAMU: (Alama 15)

Soma kifungu kifuataco kisha ujibu maswali.

Nchi nyingi duniani zimetia sahihi mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za watoto. Haki hizi ni pamoja na uhai, liseh bora inayotosha na makazi bora yaliyo salama. Hali kadhalika, kila mtoto ana haki ya kupata elimu. Elimu inastahili kutokewa bure, iwe inayofaa na inayopatikana kwa urahisi. Isitoshe, mtoto hastahili kupigwa, kudunishwa, wala kubaguliwa kwa naman yoyote ile; iwe kitabaka, kirangi, kihinsia au vinginevyo. Mtoto hapaswi kufanya kazi za kitumwa, nzito na za kushurtiswha. Vile vile, mtoto ana haki ya kutunzwa na kulindwa dhidi ya hali yoyote inayoweza kumhatirisha. Fauka ya haya, mtoto anastahili kushirikiswa katika kufanya maamuzi yanayoweza kumwathiri maishani. Pia, mtoto ana haki ya kupata huduma za afya, mahitaji maalum na habari kuhusu masuala mbalimbali. Pamoja na hayo, mtoto anastahili kupendwa na kuheshimiwa kimawazo na kihisia.

Haki za watoto zinatakiwa kulindwa na kila mwanajamii, serikali na wazazi wakiwa katika mstari wa mbele. Hii ndiyo sababy serikali za mataifa mengi zimeshiriksha haki hizi katika katiba na sheria za nchi huska. Yeyote anayezikiuka anapasa kuadhibiwa kwa mujibu wa sheria. Walakini, haki hizi bado zinakiukwa. Watoto wengi kote duniani bado wananyimwa haki zao. Kuna watoto ambao hawajawahi hata kupata kibanda cha kuweka ubavu. Wengi wa hawa wamejipata watoto ambao hawajawahi hata kupata kibanda cha kuweka ubavu. Wenig wa hawa wamejipata wakiselekea kwenye mitaa na hata majaa ya mji na vihihi ambako hulazimika kupitisha usiku hata katiak majira ya kipupwe na masika! Wengine hawapati chakula; licha ya kuwa wanatakiwa kupata chakula chenye lishe bora. Kwao kutarajia mlo awamu tatu kwa siku ni njozi; kwani hata awamu moja ni adimu kupata! La kusikitisha ni kwamba wale wanaotarajiwa kuwa vigogo wa kuzilinda haki hizi ndio wanaoongozxa katika kupalilia ukiukahi wazo. Kila siku tunasikia na kushuhudia visa vya watoto kupigwa, kushinikizwa kufanya kazi za sulubu kipunda, na kunyanyaswa kijinsia, kuishi katika mazingira hatari na hata kuuawa. Baadhi ya wanaohusika na vitendo hivi hasi huwa wazazi au jamaa wa karibu kama vile wajomba, shangazi au wahudumu wa nyumbani.

Madhila yanayowapata watoto hayatokei tu katika mazingira ya nyumbani. Mateso huvuka mipaka na kufikia ngazi ya kimataifa. Watoto wengi katika mataifa yenye fujo na ghasia hutekwa na kutumikishwa vitani. Linalokata maini ni kwamba baadhi ya viongozi katika mataifa haya hawafanyi lolote kuwanusuru. Lao huwa kuwatazama watoto wanaoktakiwa kuwalinda wakigeuzwa kuwa mababe wa kuua na kuuana. Watoto hawa huvishwa magwanda ambayo miili yao minyonge haiwezi kuyahimili. Pia hulazimika kuvaa mabuti ya kijeshi ambayo huwa nanga kwao kubeba, licha ya bunduki zinazokaribia kuwazidi uzani.

Mojawapo ya mambo ambayo viongozi nchini humu walilenga shabaha kuyafikia baada ya kujinyakulia uhuru ni elimu kwa wote. Hata hivyo, hii imekuwa kama ndoto isiyotabiirika katika baadhi ya janibu. Ni kweli kwamba sera ya elimu bila malipo katika shule za msingi nchini humu inaendelea kutekelzwa. Hata hivyo, asilimia ya watoto na hata watu wazima wasiojua kusoma na kuandika ingali kubwa. Julwaa la vijiji nchini humu na hata katika mataifa mengine ya ulimwengu wa tatu limesheheni idadi kubwa ya watoto wasioenda shuleni. Kichocheo kikuu cha hali hii ni kwamba wazazi na walezi wamejipata katika lindi la ufukara uliokithiri. Hata wanapojitahidi kujinyanyua na jujikuna wajipatapo kuyakidhi mahitaji ya kielimu ya wanoa, wao hujipata wakitapatapa katika kinamasi hicho hicho cha ulitima. Matokeo ni kwamba watoto wa matajiri wanaendelea kuelimika huku wa maskini wakibakia kwenye kiza cha ujinga. Wanaong’ang’ania kuwepo kwa elimu bila malipo ni kana kwamba ni waota ndoto mchana.

Hali ilivyo sasa hivi inadai kuwa mimi na wewe tufanye hima tuungane mikono na kutafuta suluhisho la kudumu kuhusu utekelezaji wa haki za watoto. Twapaswa kuhimiza serikali zetu kufanya kila ziwezavyo kuhakisha kuwa watoto wote wako shuleni. Nasi tushirikiane kutoa huduma kwa watoto na kukomesha dhuluma, mateso na dhiki kwao. Haitoshi kupeleka miswada bungeni kuhusu haki za watoto na kuipitisha kuwa sheria. Twastahili kubadilisha misimamo yetu kuhusu haki hizi na kuzilinda kwa dhati.

(a) Huku ukitoa mifano mine, eleza hali ya kinyume inayojitokeza katika aya ya pili. (alama 4)

………………………………………………………………………………………

………………………………………………………………………………………

………………………………………………………………………………………

………………………………………………………………………………………

………………………………………………………………………………………

……………………………………………………………………………………..

 

(b) Eleza naman hali ya usalama inavyoathiri utekelezaji wa haki za watoto kwa mujibu wa kifungu. (alama 3)

………………………………………………………………………………………

………………………………………………………………………………………

………………………………………………………………………………………

………………………………………………………………………………………

(c) kwa kurejelea aya ya nne, onyesha mchango wa serikali katika kuwajibikia haki za watoto. (alama 3)

………………………………………………………………………………………

………………………………………………………………………………………

………………………………………………………………………………………

………………………………………………………………………………………

(d) “Wanaong’ang’ania kuwepo kwa elimu malipo ni kana kwamba ni watoto ndoto mchana.” Thibitisha kauli hii kwa kurejelea kifungu. (alama 2)

………………………………………………………………………………………

………………………………………………………………………………………

………………………………………………………………………………………

(e) Eleza maana ya msamiati ufuatao kama ulivyotumika katika taarifa. (alama 3)

(i) vigogo…………………………………………………..

(ii) huwa nanga kwao………………………………………

(iii) kujikuna wajipatapo…………………………………….

2. UFUPISHO: (Alama 15)

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.

Wataalamu mbalimbali wamekuwa wakifanya utafiti kuhusu Ziwa Victoria. Juhudi hizi za uchunguzi zimekuwa zikionyesha kwamba ziwa hili ambalo ndilo la pili kwa ukubwa miongoni mwa maziwa yenye maji matamu duniani linaangamia taratibu. Inakisiwa kuwa kukauka kwa ziwa hili kutahatirisha maisha ya watu zaidi ya milioni 30 ambao hulitegemea kwa chakula na mapato. Utafiti uliofanywa na Taasisi ya Masuala ya Bahari na Uvuvi nchini ulionyshwa kuwa Ziwa Victora linagnamia kwa kiasi cha mita tatu kila mwaka. Hivi sasa baadhi ya fuo zilizokuwa kwenye ziawa hili upande wa kenay zimekauka. Manhdari ya fuo hizi nayo yameanza kutwaa sura mpya. Baadla ya kupata madau na wavuvi wakiendesha shughuli zao katika maeneo haya, huenda isiwe ajabu kupata watoto wakicheza kandanda.

Rasiimia za samaki ziwani humu zinaendelea kudidimia huku wavuvi wakitupwa kwenye biwi la umaskini. Walisema wasemo kwamba akosaye la mama hata la mbwa huamwa. Wavuvi wamebuni mikakati ya kukabiliana na hali hii ambayo inatishia kukiangamiza kizazi chao. Wengi wao wameaumua kufanya biashara maarufu kwa jina, ‘bodaboda,’ wengine wameingilia kilimo baada ya kushindwa kujikimu kimaisha kutokana na uvuvi. Wavuvi wanaoendelea kuvua samaki katika ziwa hili wamejipata katiak hali ngumu ya kiuchumi. Hali hii imewalazimisha baadhi yao kuanza kuvua samaki katika maji ya mataifa jirani; jambo ambalo limewachongea, wengi wakatiwa mbaroni huku wengine wakinyanayswa na maafisa wa usalama wa mataifa hayo jirani.

Sekta ya uchukuzi na mawasiliano nayo imeathirikasi haba. Shughuli za uchukuzi katika ziwa hili zimetignwa na gugu-maji ambalo limetapakaa kote ziwani. Mbali na gugu-maji hili, shughuli za kilimo cha kunyunyuzia maji zimetanzwa. Kadhalika, kupungua kwa viwango vya maji humu ziwani ni changamoto nyingine ambayo inawashughulisha wanaharakati wa mazingira. Inahofiwa kuwa mataifa ya Africa Mashariki yanalipoteza ziwa hili hatua kwa hatua. Hakika, wanasayansi wa masuala ya bahari wameonya kuwa ziwa hili litakauka katika kipindi cha karne moja ijayo!

Ni dhahiri kwamba jumuiya ya Afrika Mashariki ina jukumu la kulitunza ziwa hili kwa jino na ukucha. Serikali za nchi husika, hususan Kenya, Uganda na Tanzania zinapaswa kutekeleza sheria zinazodhibiti shughuli za uvuvi katika ziwa hili. Mathalan, kuna haja ya kuvua kwa misimu ili kukinga dhidi ya kuangamai kwa rasilimali za samaki. Wavuvi nao hawana buid kushauriwa kuhusu umuhimu wa kufata kanuni za uvuvi zilizowekwa na kutahadharishwa kuhusu madhara ya kuendesha uvuvi kiholela. Sheria kuhusu aina za nyavu za kuvulia pia inapaswa kutekelezwa mwa ziwa hili, pamoja na kwenye mito iliyo katika ujirani wa ziwa lenyewe. Hatua hii itasiaida kukomesha kusombwa kwa udongo na mbolea kutoka mashambani hadi ziwani. Hali kadhalika, muungano juu unapaswa kuweka sheria za kusimamia matumizi ya maji. Hili litawadhibiti raia wenye mazoea ya kubadhiri maji.

Isitoshe, serikali za mataifa ya Afrika Mashariki hazina buid kuchunguza viwanda vinavyotupa taka ndani ya ziwa hili. Mbali na kuchafua maji, viwanda hivi vinaangamiza mimea na wanyama wa majini. Uchunguzi hio unapwaswa pia kuhusisha mito inayomimina maji katika ziwa hili. Viwanda vyote vinavyotumia maji ya mito kama vile: Nzoia, Yala, Sondu-Miriu, Awach, Kuja na Kagera vinastahili kuchunbuzwa pia.

Juhudi za kufikia ustawi wa kiuchumi katika ukanda wa Afrika Mashariki zinapaswa kutilia maanani uhifadhi wa Ziwa Viktoria. Kukauka kwa ziwa hili ni sawa na kukauka kwa maazimio na ndoto zote za serikali za nchi husika za kuboresha hali ya maisha ya raia wake. Wakati ni sasa.

(a) Fupisha aya tatu za kwanza kwa maneno 70 – 75. (alama 9, 1 ya mtiririko)

Matayarisho:

………………………………………………………………………………………

………………………………………………………………………………………

………………………………………………………………………………………

………………………………………………………………………………………

………………………………………………………………………………………

………………………………………………………………………………………

………………………………………………………………………………………

………………………………………………………………………………………

Nakala safi:

………………………………………………………………………………………

………………………………………………………………………………………

………………………………………………………………………………………

………………………………………………………………………………………

………………………………………………………………………………………

………………………………………………………………………………………

………………………………………………………………………………………

………………………………………………………………………………………

(b) Huku ukitumia maneno 50 – 55, eleza masuala muhimu ambayo mwandishi anaibua katika aya tatu za mwisho. (alama 6, 1 ya mtiririko)

Matayarisho:

………………………………………………………………………………………

………………………………………………………………………………………

………………………………………………………………………………………

………………………………………………………………………………………

………………………………………………………………………………………

………………………………………………………………………………………

………………………………………………………………………………………

………………………………………………………………………………………

Nakala safi:

………………………………………………………………………………………

………………………………………………………………………………………

………………………………………………………………………………………

………………………………………………………………………………………

………………………………………………………………………………………

………………………………………………………………………………………

………………………………………………………………………………………

………………………………………………………………………………………

………………………………………………………………………………………

………………………………………………………………………………………

3. MATUMIZI YA LUGHA: (Alama 40)

(a) Huku ukitoa mfano, fafanua dhana ya mzizi wa neon (alama 2)

…………………………………………………………………………….

……………………………………………………………………………

(b) Onyesha matumizi ya kiambishi ‘Ku’ katika sentensi ifuatayo:

Amani atakutengenezea mpini wa jembe kisha aelekee kule kwao. (alama 2)

…………………………………………………………………………..

………………………………………………………………………….

(c) Andika vitamkwa vyenye sifa zifuatazo: (alama 2)

(i) Irabu ya mbele, wastani ……………………………………………

 1. Kipasuo ghuna cha kaakaa laini …………………………………

(d) Tumia kivumishi kionyeshi kisisitizi cha karibu pamoja na nomino katika ngeli ya YA – YA kutunga sentensi. (alama 2)

………………………………………………………………………………

………………………………………………………………………………

(f) Tunga sentensi yenye muundo ufuatao: (alama 2)

KN (N) + KT (T + E) + U + KN (N) + KT (T + E)

………………………………………………………………………………

………………………………………………………………………………

(g) Huku ukitoa mfano, eleza maana ya sentensi changamano. (alama 2)

………………………………………………………………………………

………………………………………………………………………………

(h) Tunga sentensi moja kutofautisha maana ya: koga na konga. (alama 2)

………………………………………………………………………………

………………………………………………………………………………

(i) Tunga sentensi moja yenye nomino dhahania na nomino ya jamii (alama 2)

………………………………………………………………………………

………………………………………………………………………………

(i) Nyamuba vitenzi vifuatavyo katika kauli zilizo kwenye mabano. (alama 3)

(i) nywa (tendesha) ………………………………………………………

 1. la (tendeana) ……………………………………………………………
 2. vaa (tendwa) ………………………………………………………….

(k) Akifisha sentensi ifuatayo kubainish dhana tatu tofauti.

Julius Kiptoo mwanawe Kung’u na Justine walikiletea kijiji chao sifa. (alama 3)

………………………………………………………………………………

………………………………………………………………………………

………………………………………………………………………………

………………………………………………………………………………

(l) Ainisha manenoyaliyopigwa mstari.

Naam, ameleta machache (2 marks)

…………………………………………………………………………….

(m) Tunga sentensi yenye kitenzi kishirikishi kikamilifu. (alama 2)

…………………………………………………………………………………….

……………………………………………………………………………………..

(n) (i) Eleza maana ya shadda. (alama 1)

……………………………………………………………………………………

(ii) Onyesha panapotokea shadda katika neon: ‘mteremko’. (alama 1)

………………………………………………………………………………………

(o) Andika visawe vya maneno yaliyopigwa mstari. (alama 2)

Sahibu ya alishikwa na kisunzi.

………………………………………………………………………………………

(p) Bainisha aina za virai vilivyopigwa mistari.

Ubaguzi wa kijinsia umekshifiwa na viongozi wenye misimano tahbiti mno (alama 3)

……………………………………………………………………………………

…………………………………………………………………………………….

(q) Andika sentensi ifuatayo katika usemi wa taarifa.

“Shughuli yetu itamalizika kesho,” mama alimwambia Juma. (alama 2)

……………………………………………………………………………………

…………………………………………………………………………………….

(r) Bainisha kiima na chagizo katika sentensi ifuatayo:

Watahiniwa hao walisoma maswali yote kwa makini. (alama 2)

……………………………………………………………………………………..

(s) Ainisha sentensi ifuatayo kwa kuzingatia jukumu/dhamira yake.

Funga majani matano matano kwa kila fungu. (alama 1)

…………………………………………………………………………………..

4. ISIMU JANII (Alama 10)

Eleza kwa ufupi jinsi mambao yafuatayo yanovyodhibiti mitindo ya lugha.

(a) Mazingira (alama 4)

……………………………………………………………………………………

…………………………………………………………………………………….

……………………………………………………………………………………

…………………………………………………………………………………….

……………………………………………………………………………………

…………………………………………………………………………………….

(b) Madhumuni (alama 2)

……………………………………………………………………………………

…………………………………………………………………………………….

…………………………………………………………………………………….

(c) Malezi (alama 4)

……………………………………………………………………………………

…………………………………………………………………………………….

……………………………………………………………………………………

…………………………………………………………………………………….

……………………………………………………………………………………

…………………………………………………………………………………….

102/3

KISWAHILI

Karatasi ya 3

FASIHI

Okt./Nov. 2012

Muda: Saa 2 ½

THE KENYA NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL

Kenya Certificate of Secondary Education

KISWAHILI

Karatasi ya 3 102/3 Kiswahili P3 – Fasihi

FASIHI Friday 11:00 am – 1:30 pm

Muda: Saa 2 ½ 09/11/2012 (2nd Session)

Maagizo

 1. Jibu maswali manne pekee
 2. Swali la kwanza ni la lazima
 3. Maswali hayo mengien matatu yachaguliwe kutoka sehemu nne zilizobaki; yaani:

Riwaya, Tamthilia, ushairi na Fasihi simulizi

 1. Usijibu maswali mawili kutoka sehemu moja
 2. Karatasi hii ina kurasa 6 zilizopigwa chapa
 3. Watahiniwa ni lazima wahakikishe kwamba kurasa zote zimepigwa chapa sawasawa na kuwa maswali yote yamo.

SEHEMU A: HADITHI FUPI

K.W. Wmitila: Mayai Waziri wa Maradhi na Hadithi Nyingine

1 (a) Eleza nafsi ya usimuliz iliyotumiwa katika hadithi ya “Mkimbizi”. (alama 3)

(b) Bainisha mifano mitatu ya mbinu rejeshi katika hadithi hii na ueleze umuhimu wa kila mojawapo. (alama 8)

(c) “Ukimbizi ni kikwazo cha maendeleo.” Thibitisha kauli hii kwa kurejelea hadithi hii. (alama 8)

SEHEMU B: RIWAYA

Said A. Mohamed: Utengano

Jibu swali la 2 au la 3.

2. ‘Lo, ana wewe mchawi,… Cheleko …nakuvisha kilemba.’

(a) Fafanua muktadha wa donodoo hili (alama 4)

(b) Andika tamathali mbili za usemi zinazojitokeza katika dondoo hii. (alama 4)

(c) ‘Wewe mchawi.’ Onyesha jinsi kauli hii inavyomwafiki muzngumziwa kwa kurjelea riwaya. (alama 12)

3. “Wanawake katika Utengano ni vyombo vikuu vya ukiukaji wa haki za kibanadamu.” Thibitisha. (alama 20)

SEHEMU C: TAMTHILIA

Kithaka wa Mberia: Kifo Kisimani

Jibu swali la 4 au la 5

4. “Mtukugu mtemi anafurahia sana .. Kama ujuavyo, anapenda sana watoto… Kwa hakika, kama mzazi, hana kifani katika Butangi nzima.”

(a) (i) Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)

(ii) Taja na utoe mfano wa sifa moja ya mzungumzaji inayojitokeza dondoo hili. (alama 2)

 1. Fafanua vichocheo vine vya sifa uliyotaja katika (ii) hapa juu. (alama 10)

5. “Anwani” ‘Kifo Kisimani’ inaafiki tamthilia hii. Thibitisha. (alama 20)

SEHEMU D: USHAIRI

Jibu swali la 6 au la 7

6. Soma shairi lifuatalo kasha ujibu maswali

Said A. Mohamed: Mbele Ya Safari

1. Ilipoanza safari, iianza kwa dhiki 5. Msafara ukasita, kwenye mlima wa haki

Tulishikana kwa ari, kwenda safari ya haki Kijasho kinatuita, mlima haupandiki

Tukawa ni majabari, nyoyo zisitaharuki Basi sote ‘kajipeta, kukikwea kima hiki

Tukajizatiti Twataka hazina

2. Njaa ikawa thabiti, na kiu kutamalaki 6. Tukiwa migongo wazi, tukainama kwa shaki

Nais tulitia dhati, tusijali kuhiliki Tukawa’ chia ukwezi, kialeni wadiriki

Ingawa mbele mauti, dhila na migni mikiki Wakapanda bila kazi, kuteremsha miliki

Tulijizatiti Wakaitapia.

3. Huu mwisho wa safari, tukaambiwa ni haki 7. Wakafikia makazi, ya pumbao na ashiki

Shangwe kwetu na fahari, utumwa hatuutaki Huko wakajibarizi, kwenye raha lakilaki

Kuwa mbele ya safari, juhudi iliyobaki Wakaisahau ngazi, ya umma ulomiliki

Kuwa mbel ya safari, juhudi iliyobaki Wakaisahau ngazi, ya umma ulomiliki

Tulijizatiti Mbele ya safari

4. Ile ilikuwa ndoto, mwisho wake mafataki 8. Na hazina yetu sote, kuishusha hawataki

Nguvu zimechomwa moto, sahala ‘mekuwa dhiki Wamo wanatema mate, kwa umati halaiki

Wagombania kipato, utashi haukatiki Imezima nia yote, kiza hakitakasiki

Na kutabakari Mbele ya safari

(a) Eleza safari inayorejelwa katika shairi hili. (alama 2)

(b) Onyesha kinaya cha safari inayozungumziwa. (alama 6)

(c) Taja na ueleze bahari mbili za shairi hili ukizingatia: (alama 4)

 1. mizani;
 2. vina

(d) Andika ubeti wa saba kwa lugha ya nathari (alama 4)

(e) Eleza umuhimu wa aina mbili za uhuru wa kishairi zilizotumiwa katika ubeti wa sita. (alama 4)

7. Soma shairi lufuatalo kasha ujibu maswali

1. Wakati tunywapo chai hapa upenuni 4. Sasa tukisubiri ndoto tusizoweza kuzitekeleza tena

Na kuwatazam watoto wetu Tumalizie machicha ya chai yetu ya jioni

Wakicheza bembea kwa furaha Bila ya kutematema na kwa tabasamu

Tujue kamba ya bembea yetu imeshalika Na baada ya hapo tujilambe utamuutamu

Na bado kidogo tutaporomoka Uliobakia kwenye midomo yetu

2. Kulikuwa na wakati ulinisukuma juu 5. Tukikumbuka siku ilee ye kwanza

Nikaenda ziadi ya nusu duara Tulipokutana jioni chini ya mwembe

Kulikuwa na wakati nilikudaka Tukitafuta tawi zuri gumu

Ulipokaribia kuanguka La kufunga bembea yetu

Na kulikuwa na wakati tulibebana kwa zamu Naye mbwa Simba akisubiri

3. Wakati huo, japo tulipaa mbele na nyuma 6. Lakini kabla hatujaondoka kimyakimya

Tulicheka kwa matumaini yaliyotiwa chumvi Kukamilisha nusu duara iliyobaki

Na kisha tukaongozana jikoni kupika chajio Tuhakikishe vikombe vyetu ni safi

Ilikuwa adhuhuri yetu Tuhakikishe vikombe vyetu ni safi.

(E. Kezilahabi)

(a) Fafanua maana ya kijuuujuu na maana ya kitamathali ya shairi hili. (alama 6)

(b) Bainisha matumizi ya vipengele vifuatavyo katika shairi: (alama 6)

 1. Usimulizi;
 2. Usambamba;
 3. Taswira

(c) Tambulisha mzungumzaji (nafsi – neni) katika shairi hili. (alama 2)

(d) Fafnua toni ya shairi hili (alama 4)

(e) Eleza maana ya mshororo: “Tuhakikishe vikombe vyetu ni safi.” (alama 2)

SEHEMU E: FASHIHI SIMULIZI

8. (a) Huku ukitoa mifano, fafanua majukumu matano ya nyimbo (alama 10)

(b) “Mwimbaji ana nafasi muhimu katika kufanikisha uwasilishaji wa wimbo.”

Thibitisha. (alama 10)

HUU NDIO UKURASA WA MWISHO ULIOPIGWA CHAPA