KNEC kiswahili 2011 Exam past papers

Exam year:2011

High school past papers

MWAKA WA 2011

KARATASI YA 1

1 Jnsha ya lazima,

Wewe kama mwanaiimzi uraepata nafasi ya kumhoji Mkurugenzi wa Haban nchini kuliusu umuhimu wa magazeti kwa wanafiinzi washule za sekondari. Andika mahojiaao hayo.

2 “Magari ya matatu yameleta faida nyingi Kapa nchini kuliko hasara.” Tadili.

3 Pele hupewa msi kucha.

4 Andika insha itakayomalizika kwa:

“Niliipapia ile bilauri ya maji kwa pupa. Sikuwa na uhakika kuwa kiu yangu ingekatika.
Nikapiga mafunda mawili, matatu. Baada ya kugumia-bilauri yote, ndipo nilipotambua kuwa
kweli maji ni uhai.”

KARATASI YA 2

UFAHAMU (Alama l5)

Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali.

Changamoto kubwa inayowakabili watu wengi katika mataifa yanayoendelea ni suala la chakula. Suala hii linaweza kuangaliwa katika sawia mbili tofauti. Kuna tatizo linalofungamana na uhaba wa chakula chenyewe. Uhaba huu unaweza kutokana na utegemezi mkubwa kwa zaraa kama nyenzo kuu ya uzalishaji wa chakula.

Zaraa katika malaifa inengi hususan yanayoendelea, hutegemea mvua. Kupalikana kwa mvua huathiriwa na mabadiliko ya tabianchi ulimwenguni. Malendo na amali za waLu kama ukataji wa miti na uchafuzi wa mazingira huwa na alhari hasi kvvcnye tabianchi hiyo. MabadilJko ya tabianchi huweza kuvyaza ukame kutokana na ngambi ya mvua.

Kibinimethali hutokea wakati mafuriko yanapotokea na labda kuyasomba mazao mashambam na kusababisha baa la njaa. Hali hizi mbili husababisha matatizo makubwa ya chakula na kuathiri pakubwa suala zima la usalama wa chakula. Tli kuzuia uwezekano wa kuwepo kwa shida hii, pana haja ya kuwepo kwa mikakati na sera za kuhakikisha kuna usalama wa chakula, Kwa mfano, pana haja ya kukuza kilimo cha umwagiliaji ili kuepuka adha ipayosababishwa na ukosefu wa mvua. Kwa upande mwingine, sharti zichukuliwe hatua mufidi za kuzuia na kupambana na alhari za gharika.

Changamoto nyingine inahusiana na usalama wa chakula chenyewe. Chakula kilichosibikwa na vijasumu au kwa njia nyingine lie huweza kumdhuru anayehusika. Msibiko wa chakula unatokana na vyanzo tofauti. Mathalan, uandalizi wa chakula kilichochafuliwa na choo, kulozingalia mbeko za usafi, uandaaji wa chakula na kukiweka katika liali ya uvuguvugu kabla ya kukipakua hali inayochoehea ukuaji wa viini na ulaji wa chakula kisichoandaliwa vyema.

Hi kuepuka uwezekano wa kuadhirika, pana haja ya kuzingatia usafi wa chakula na uandalizi unaofaa. Fauka ya hayo, vyombo vya uandalizi viwe sail, kanuni za usafi zlfuatwe, upikaji na uandaaji uwe kamilifu. Hali hii isipozingatiwa, siha za raia wenyewezitaathirika pakubwa.

Maswali

(a) Taja aina mbili za kuangalia suaJa la chakula katika mataifa yanayoendelea. (alama 2)

(b) Taja hatua mbili zinazoweza kuchukuliwa kupambana na tatizo la chakula. (alama 2)

(c) Eleza jinsi nne tofauti namna chakula kinavyoweza kuwa si salama? (alama 4)

(d) Kwa nini inahalisi kukipakua chakula baada ya kukiandaa tu? (alama 1)

(e) Ni mapendekezo gani anayoyatoa mwandishi kuhakikisha kuwa chakula kinafaa?

(alama 4)

(f) Eleza maana ya maneno haya jinsi yalivyotumiwa: (alama 2)
(i) Ngambi yamvua ………………………………………………………………………..’…………….

(ii) Adha……………………………………………………………………………………………………….

MUKTASARI

Uwazaji tunduizi ni tendo ambalo huhusisha matumizi ya akili. Uwazaji huu umekitwa kwenye matumizi ya michakato kama makini, upangiliaji, uteuzi na tathmini. Hata hivyo, uwazaji huu si mchakato mwepesi bali ni mchakato changamano.

Mchakato wa uwazaji tunduizi unahusisha stadi na mikabala tofauti. Mathalan, kuweza kutambua na kubainisha misimamo ya watu wengjne, hoja wanazozua na uamuzi waliofikia, kutathmini au kupima ushahidi uliopo ili kubainisha mitazamo tofauti. Vilevile, uwazaji tunduizi hushirikisha kupima hoja za upinzani na ushahidi uliopo kwa njia ya haki pamoja na kutambua yaliyofichwa au ukweli uliofunikwa na taswira ya juu juu, Hali kadhalika, uwazaji tunduizi hujumuisha kutambua mbinu zinazotumiwa kufikia misimamo fulani kwa mvuto zaidi na kwa matumizi ya mbinu za kishawishi. Aidha, uwazaji huu huhitaji kutathmini masuala kwa mtindo ulio wazi, kufikia uamuzi kama hoja zinazotumiwa zina mashiko au zinakubalika kuwa nzuri. Zaidi ya hayo, uwazaji tunduizi unahusisha kuwasilisha mtazamo kwa njia yenye uwazaji mzuri na inayoshawishi.

Uwazaji tunduizi una manufaa anuwai. Mosi, unasaidia kujenga makini ya utendaji. Pili, hupevusha uwezo wa usomaji kwa kuufanya usomaji huo uwe na malengo wazi, Fauka ya hayo, unamsaidia mtumiaji kutambua hoja kuu katika malini au ujumbe fulani bila ya kuzongwazongwa na hoja duni za pembeni. Uwazaji huu unasaidia kuuchonga uwezo wa kuikabili au kuiitikia hali fulani na kukuza stadi za uchanganuzi. Mwanadamu huwa. mtu tofauti na bora anapoujenga na kuuimarisha uwazaji tunduizi wake.

Maswali

(a) Bila kubadilisha maana aliyokusudia mwandishi, fupisha aya mbili za mwanzo.

(Maneno 70-80) (alama 10; alama 2 za utiririko)
Matayarisho:

Nakala safi:

(b) Andika kwa muhtasari mambo muhimu katika aya ya tatu. (Maneno 35 – 40)

(alama 5; alama 1 ya utiririko)

Matayarisho:

Nakala safi:

3 MATUMIZI YA LUGHA.

(a) Tumia mzizi ‘- enye’ katika sentensi kama:

(i) Kivumishi …………………………………………………………………………………………………

(ii) Kiwakilishi ……………………………………………………………………………………………….

(alama 2)

(b) Andika sentensi ifuatayo katika ukubwa:-

Paka mweupe amenaswa mguum. (alama 2)

(c) Taja mfano mmoja mmoja wa sauti zifuatazo:-

(i) Kiyeyusho………………………………………………………………………………………………..

(ii) Kimadende………………………………………………………………………………………………..

(alama 1)

(d) Onyesha shamirisho kitondo, kipozi na ala katika sentensi iluatayp:-Kipkemboi alimbebea mwalimu mzigo kwa gari. (alama 3)

(e) Changanua sentensi ifuatayo kwa kutumia jedwali.

Maria alipika taratibu huku mama akimwelekeza vizuri. (alama 4)
…………………………………………………………………………………………………………………………..

(f) Nomino ‘furaha’ iko katika ngeli gani?

…………………………………………………………………………………………………………. (alama 1)

(g) Andika kinyume cha sentensi:

Watoto wameombwa waanike nguo. (alama 2)

(h) Andika sentensi ifuatayo upya kwa kufuata maagizo uliyopewa. Mama alishangilia arusi ya mwana. Anza: Mwana …………………………………………………………………………………….. (alama 2)

(i) Tumia kifejeshi ‘0’ kalika sentensi ifuata’yo:-

Mtu arabaye hutupa tope hujichafua mweny’ewe. (alama 2)

(j) Kanusha sentensi ifuatayo:

Mgonjwa huyo alipona na kurejea hyumbani. (alama 2)

(k) Ainisha vihusishi katika sentensi:

Ame aliwasili mapema kuliko wengine halafu akaondoka. (alama 2)

(1) Tunga sentensi mbili kuonyesha maana tofauti za neno “chuma”. (alama 4)

(i) ……………,……………….

(ii) ………………………………………………………….

(m) Undauomino kutokana nakitenzi ‘tafakari’…………………………………………. (alama 1)

(n) Eleza maana mbili za sentensi:

Tuliitwa na Juma ………………………………………………………………………………. (alama 2)

(o) Ainisha viambishi katika kitenzi:-

Tutaonana…………………………………………………………………………………… (alama 2)

(p) Tunga sentensi rnoja ukiturnia kiunganishi cha kinyume.

(q) Huku ukitoa mifano eleza miundo. miwili ya silabi za Kiswahili. (alama 2)

 

(r) Akifisha kifungu kifuatacho: –

Mzee alimwambia mwanawe njop nikupeleke kwa babu yako angalau umjue

mtoto aliuliza nani babu? . (alama 4)

ISIMUJAMII

(a) Bainisha changamoto tano zinazoikabili lugha ya Kiswahili kama somo katika shule za upili nchini Kenya. (alama 5)

(b) Eleza namna tano za kukabiliana na changamoto ulizobainisba hapo juu. (alama 5)

KARATASI 3

SEHEMU A: TAMTHILIA

KlTHAKA WAMBERIA: Kifo Kisimani

Swali la lazima

“Alijiona pwagu. Laldni Butangi ina pwaguzi pia.”

Eleza tofauti baina ya wahusika wanaorejeldwa. (alama 20)

SEHEMU 6: RIWAYA

S.A. MOHAMED: Utengano Jibu swali la 2 au la 3

2 Eleza namna mbinu zifuatazo zilivyotumiwa na mwandishi wa riwaya ya Utengano:

Kwelikinzani

Sadfa. (alama 20)

“Uhuru alioutaka na ulimwengu alioufahamu Maimuna umemdhuru hatimaye.”

Thibitisha kauli hii kwa kutoa mifano kumi. (alama 20)

SEHEMU C: USHAIRI

Jibu swali la 4 au la 5

KUJITEGEMEA

1 Nchi ni ile ambayo, imekita ardhini 3 Twaishije tujihoji, wanachi humu nchini

Siyo ile iombayo, ghaibu na majirani Kila tunachohitaji, kupatakwe ugenini

Taratibu siyo hiyo, wanachi twambizaneni Hiyo ni tete haviji, tongo tupangusaneni

Daima hukaa chini, maganja ya mpewaji Daima hukaa chini, maganja ya mpewaji

2 Chumo lote na mitaji, leo lirao maganjani 4 Kuomba wataalamu, ni mwendo hauh’ngani

Bepari na wanyonyaji, wasalie maguguni Tupate wa humu humu, wajuzi wa kila fani

Shime utekelezaji, vingine havifanani Mbele washike hatamu, kwa mapimo na makini

Daima hukaa chini, maganja ya mpewaji Daima hukaa chini, maganja ya mpewaji

5 Tuufuate wongozi, pamwe na nyingi imani 6 Vote hatuyatimizi, alotimiza ni nani

Tushiriki kila kazi, na mambo yalomkini Lakini tuwe maizi, tusizurure mijini

Mikopo ina kinyezi, si kitu cha tumaini Tbkamshabihi kozi, kipanga au kunguni

Daima hukaa chini, maganja ya mpewaji Daima hukaa chini, maganja ya mpewaji

7 Shujaa itakiwavyo, aonekane vitani

Nasisi vita tunavyo, roho kwa roho ugani

‘Kutegeniea’ vilivyo, kondo tujiamueni
Daima hukaa chini, maganja ya mpewaji

Boukhet Amana: Malenga wa Mrima

Mwinyihatibu Mohammed Oxford University Press

1977

  1. Mtunzi wa shairi hili ana dhamira gani? (alama 2)
  2. Shairi hili ni la aina gani? Tea sababu moja. (alama 2)
  3. Eleza mambo matatu ambayo mshairi anashauri nchf ifanye ili kujitegemea. (alama 3)
  4. Taja aina moja ya idhini ya kishairi iliyojitokeza kwa wingi zaidi katika shairi na utoe mifano mitano ya matumizi yake. (alama 7)
  5. Andika ubeti wa pili kwa lugha ya nathari. (alama 4)
  6. Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumiwa katika shairi:
  7. Ghaibu
  8. Tukamshabihi. (alama 2)

 

HAKI

1. Haki watutisha, tusikuandame, kwa matendo yetu, Watukorofisha, tusikuandame, kila penye kitu, Mbona watugwisha, miba ituchome kwenye huu mwitu, Tutokwe na utu!

2. Hatutakufanya, mwana kwa mvyele; aliyemzaa,

Haki watunyima, machumi ya mbele, na nyingi hadaa, Tuchumayo nyanya, uchungu umbele, hatuna wasaa, Haki twashangaa! :

3. Na kambi nzima, kunaiyenea, hasa hapa petu, Tunakutazama, kwa kuulizia, kuweza thubutu, Na kwenye milima, ilotueka, kupandia watu, Usifanyekatu!

4. Sio hao mabwana, waloteuliwa, kupata mwangaza, Haki wakubana, lilotarajiwa, kwenye hichi kiza, Ndevu kuchomana, wengine kuliwa, tukijiingiza, Kambi yatuviza!

5. Haki buna njia, kizuizi mali, ndio njia panda, Tukiifatia, hatufiki mbali, wengi tunaganda, Sio yetu nia, lakini akili, mali ishapenda, Haki yatuponza!

6. Wala hutasemwa, sababu ni nyoyo, kwisha haribika,

Ya mali kuchumwa, vyovyote iwavyo, itavyopatika, Wakati mtumwa, ushatumwa ndivyo, na ushatufika, Kwetu nimashaka!

7. Haki hufanyiki, papitapo mambo, na vikubwa visa, Watu hawataki, kutenda kijambo, tunu yao pesa, Sisi kwetu dhiki, yatunisha tumbo, wao hata hisa, Nandio yasasa!

Haki husimami, kwa viumbe sisi, tuvyojaaliwa, Na huna ulimi, kuweza tukisi, tukageukiwa, Zama za uchumi, zishashika kasi, nguvu zishapewa, Haki wauliwa!

9. Iwe hivi haki, hakuna mmoja, akukumbukae,

Hatuna ashiki,kuvutalahaja,haki ituvae,

Mbona hatutaki, twalia na tija, haki iambae,

Haki tamati!

Suleiman A. All:

Malenga Wapya

(a) Eleza dhamira ya shairi hili. ; (alama2)

(b) Huku ukitoa mfano, eleza aina ya shairi hili. (alama 3)

(c) Taja na ufafanue tamathali ya usemi inayotawala katika shairi hili. (alama 3)

(d) Kwa kutoa mfano mmoja mmoja, onyesha aina tatu za idhini ya kishairi katika shairi hili.

(alama 6)

(e) Andika ubeti wa saba kwa lugha ya nathari. (alama 4)

(f) Mshairi ana maana gani kwa kusema:

(i) Kambi yatuviza

(ii) Kuweza tukisi. (alama 2)

SEHEMU D: HADITHI FUPI

K.W. WAMITILA: Mayai Waziri Wa Maradhi na Hadithi Nyinginezo

Jibu swali la 6 au la 7

6 “Cheche ndogo hufanya moto mkubwa.”

(a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)

(b) Fafanua niaudhui manne yanayohusiaha na chanzo cha tukio Hnalorejeiewa katika dondoo hilo. (alama 8)

(c) Eleza matokeo manne ya tukio linalorejelewa katika dondoo. (alama 8)

7 “Mganga na wateja wake wote walikosa busara.” Fafanua ukweli wa kauli hii kwa raifano kumi kutoka hadithi ya ‘Siku ya Mganga/

(alama 20)

SEHEMU E: FASIHI SIMULIZI

8. (a) Eleza maana ya malumbano ya utani. (alama 2)

(b) Bainisha sifa nne za malumbano ya utani. (alama 8)

(c) Fafanua majukumu matano ya malumbano ya utani katika jamii. (alama 10)

More High School Past Papers